Polisi wachunguza kisa cha moto Bamburi.


Polisi hapa mjini Mombasa wameanzisha uchunguzi dhidi ya kisa cha moto ulioteketeza sehemu ya klabu ya burudani ya Masters Club ilioko Bamburi mjini Mombasa hapo jana jioni.

Afisa mkuu wa polisi kisauni Julius Kiragu amesema kwamba chanzo cha moto huo hakijabainika huku uchunguzi kubaini chake ukianzishwa.

Hata hivyo hakuna aliyeripotiwa kujeriwa kwenye mkasa huo wa moto uliotekereza kabisa sehemu ya klabu hio iloyoezekwa makuti.

Haijabainika iwapo kunao watu waliokuwa wakihudumu kwenye klabu hio kinyume cha sheria kwani serikali ilikuwa tayari imepiga mafuku huduma za vilabu na bar zote kwenye kaunti ya Mombasa.

Imewachukua kikosi cha wazima moto na maafisa wa kukabiliana na majanga muda wa masaa mawili kabla kuuzima kabisa moto huo unaodaiwa kusababisha hasara ya kiwango ambacho hakijabainika.