POLISI NA UCHUNGUZI WA KISA CHA MWANAMUME ALIYEPATIKANA AMEJITIA KITANZI-MOMBASA.


Polisi katika eneo bunge la Nyali hapa mjini Mombasa wanachunguza kisa cha mwanamume mmoja ,aliyepatikana amejitia kitanzi katika mojawapo ya nyumba aliyokuwa akihudumu kama seremala, katika mtaa wa Matopeni kule Kongowea kaunti hii ya Mombasa.

Kulingana na afisa mkuu wa polisi katika eneo bunge la Nyali Daniel Masaba, mwili wa mwanamume huyo ulipatikana ukining’inia kwenye kamba iliofungwa katika paa ya nyumba hio, ambayo ni sehemu ya kutengeneza vitanda na viti.

Mmiliki wa sehemu hiyo ambaye pia ni mwajiri wa marehemu anasema kwamba ,marehemu alikuwa buheri wa afya hapo jana hadi akafunga kazi na kwenda nyumbani, na haijabainika ni kwanini aliregea kazini na kuamua kujitoa uhai.

Polisi wanasema kwamba uchunguzi uliofanyiwa mwili wake umebaini kwamba ,hakuwa na alama zozote za majeraha mwilini na wala hakuacha taarifa yoyote kabla ya kuchukua hatua hio, kwani alikuwa akiishi peke yake.