Polisi Migori wachunguza kifo tatanishi cha mwanamume


Polisi eneo la Suna Mashariki kaunti ya Migori wameanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na kifo cha mwanamume wa umri wa miaka 77 aliyepatikana ameafariki dunia baada ya kupotea katika kijiji cha Hollo kata ya Onguo Suna Rabuor kaunti ya Migori.

Chifu wa eneo hilo Philip Kisiagro anasema kuwa Joseph Nyandege alipatikana mapema leo akiwa ameaga dunia hatua chache kutoka nyumbani wkake, siku moja baada ya kuripotiwa kutoweka.

Chifu huyo anasema kuwa kichwa cha marehemu kilikuwa na matone ya damu ishara kuwa huenda aliuawa kwingine na mwili wake kutupwa eneo hilo.

Mwili wa mareehmu umelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Migori level 4 uchunguzi zaidi ukiendelea.