Polisi ashtakiwa kwa kumuua mtoto


Afisa wa polisi Duncan Ndiema amekanusha mashtaka ya kumuua mvulana wa umri wa miaka 13 Yassin Moyo katika eneo la kiamaiko hapa jijini Nairobi.

Jaji wa mahakama kuu Luka Kimaru ameagiza Mshukiwa aendee kuzuiliwa na polisi mahakama ikitarajiwa kusikiza ombi lake la kutaka kuachiliwa kwa dhamana hapo kesho.

Mshukiwa alikosa kujibu mashtaka juma lililopita baada ya wakili wake Danstan omari kuambia mahakama kuwa alikuwa katika hospitali ya Mbagathi akionyesha dalili za ugonjwa wa Covid-19 lakini leo mahakama imeambiwa kuwa hana ugonjwa huo.