Oparesheni ya wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza yaendelea Lamu.


Naibu kamishna eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu Emanuel Koech ametoa wito kwa wakaazi eneo hilo kuona kwamba wanawao wanaenda shuleni kama vile ilivyoamriwa na serikali ya kitaifa.

Kulingana na Koech atakama wanafunzi wamefeli katika masomo yao ya darasa la nane ni sharti wanafunzi hao waende shuleni haijalishi alama gani wamepata katika mtihano wao wa kitaifa KCPE

Amesema kulingana na mpango wa serikali kuu mwanafunzi wa darasa la nane anapofeli KCPE hapaswi kuregelea shule ya msingi na kwamba mwito ni wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza.