ONYO BAADA YA WAHANGA WA MAFURIKO KUANZA KUJENGA


Onyo kali limetolewa kwa wahanga wa mafuriko ya mwezi disemba mwaka jana dhidi ya kuanza kujenga upya nyumba zao karibu na mto Voi.
Kulingana na Mwakilishi wodi ya Kaloleni Omar Ahmed amesema serikali ya kaunti haitovumilia wahanga hao kujenga upya karibu na mto huo kwani huenda wakakubwa na mafuriko kutakaponyesha tena.
Omar aidha amesema kwamba serikali ya kaunti itaendelea kutafuta ardhi mbadala ili familia 40 zilizokumbwa na mafuriko zipate makao mapya.