Nzige wazimwa Marsabit


Wizara ya kilimo katika Serikali ya kitaifa ikishirikiana na serikali ya kaunti ya Marsabit imeanza kunyunyia dawa ya kuangamiza Nzige ambao wamevamia sehemu kadhaa kaunti hiyo ya marsabit.

Shughuli hiyo ya juma moja imeanza kutekelezwa leo katika eneo la North Horr ambalo limeathirika Zaidi na wadudu hao.

Ndege mbili za kunyunyiza dawa pamoja na nyingine moja kutoka shirika la huduma kwa wanyama pori nchini KWS zinanatekeleza zoezi hilo katika maeneo yaliyoathirika kwa mjibu wa maafisa wa wizara ya kilimo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shughuli hiyo katika uwanja wa ndege mjini Marsabit, gavana Mohamud Mohammed Ali, amesema kwamba maeneo kadhaa ya kaunti yameathirika kutokana na wadudu hao.

Anasema kwamba kaunti zote ndogo zilishuhudia wadudu hao ikiwemo Moyale, Saku, Laisamis na kwa sasa wadudu hao wako kule North Horr.