Nyumba zaathirika na mafuriko Lamu.


Zaidi ya nyumba 500 katika kaunti ya Lamu zimeathirika na mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazonyesha maeneo ya nyanda za juu ambayo imesababisha Mto Tana kuvunja kingo zake kaunti ya Tanariver na hatimaye kusababisha mafuriko hayo.

Mshirikishi wa shirika la Msalaba Mwekundu kaunti ya Lamu Kawthar Alwy amesema maeneo yaliyoathirika Zaidi na mafuriko hayo ni Amkeni,Maandani,Marafa,Lumsh,Chalaluma akisema ni maeneo yanayopakana na mto sawa na ziwa.

Alwy ametoa wito kwa wakaazi ambao wako katika sehemu za chini zilizokwenye athari ya kumbwa ya kusombwa na mafuriko kuhama maeneo salama ya juu ili kuepukana kusombwa na mafuriko.

Haya yanajiri huku mvua kubwa zikiendelea kunyesha katika maeneo mengi ya kaunti ya Lamu huku wakulima wakiendelea kukadiria hasara baada ya mimea yao kusombwa na maji.