NHIF kusaidia gharama ya wagonjwa wa COVID 19 Lamu.


Familia zaidi ya elfu 20 zilizosajiliwa kuwa na kadi ya Bima ya NHIF katika kaunti ya Lamu ili kupokea matibabu ya bure,zitaweza kunufainika pia na matibabu ya bure iwapo wamepata maambukizi ya virusi vya korona.

Gavana wa kaunti ya Lamu Fahim Twaha amesema mwananchi yoyote aliyesajiliwa kadi ya NHIF Lamu pindi anapopata virusi vya korona kadi hiyo itamugharamikia matibabu yake katika hospitali zilizosajiliwa na wizara ya afya nchini.

Kulingana na Gavana Twaha hatua hiyo inalenga kuwapunguzia mzingo wakaazi wa Lamu ambao wengi ni maskini hawawezi kumudu maisha yao.

Twaha amesema katika hospitali zote kaunti ya Lamu kuna vitanda 30 vya kuwalaza wagonjwa wa korona,huku serikali yakle ikiwa na mipango ya kununua vitanda vya ICU.

Kufikia sasa Lamu imeweza kupima watu 441ili kubaini iwapo wameathirika virusi vya korona miongoni mwao watu 26 wamepatikana na virusi hivyo.