NHIF kuanza kugharamia Covid-19


Ni afueni kwa wakenya baada ya wasimamizi wa Hazina ya kitaifa ya bima ya afya NHIF kutangaza kuwa bima hiyo itagharamia matibabu ya ugonjwa wa Covid-19.

Kupitia taarifa, afisa mkuu msimamizi wa NHIF Peter Kamunyo amesema kuwa bima hiyo itasimamia wamiliki wake sawa na wanaowategemea katika hospitali za umma zilizo chini ya wizara ya afya.

Hospitali hizo ni pamoja na hospitali ya kitaifa ya Kenyatta, Hospitali ya mafunzo na rufaa ya Chuo kikuu cha kenyatta na Mbagathi.

Hospitali zingine ni zilizo maeneo ya kaunti.