NET ZA MBU KUGAWANYWA MOMBASA


Kaunti ya Mombasa inatarajia kuanza kugawa neti za kujikinga na mbu laki 7 na elfu 60 katika juhudi za kupunguza visa vya ugonjwa wa malaria.

Hatua hii ni katika kupigana na ugonjwa huo.
Hamasa na usajili watakaonufaika mashinani utaanza ili kuhakikisha hakuna jamii inaachwa nyuma kwenye zoezi hilo.

Haya yanajiri huku maeneo ya Likoni na Kongowea katika kaunti ya Mombasa yakiwa miongoni mwa sehemu zilizoripoti visa vya juu vya ugonjwa huo.

Wizara ya afya nchini inapania kupeana neti millioni 15.7 ambazo zimetibiwa katika kaunti 27 kote nchini.