NCCK yatilia shaka ‘zawadi’ kwa MCAs


Baraza la kitaifa la makanisa nchini NCCK limeelezea kutoridhishwa na hatua ya serikali ya kuwatengea waakilishi wadi nchini mgao wa pesa za magarai wanapojadili mswada wa mabadiliko ya katiba kupitia BBI.

Baraza hilo likiongozwa na katibu mkuu askofu chris kinyanjui linasema kuwa hatua hiyo iko sawa lakini imetekelezwa wakati usiofaa.

Licha ya hayo baraza hilo limehimiza mabunge ya kaunti nchini kuhusisha wananchi kikamilifu katika kujadili mswada huo.

Baraza hilo pia linashinikiza makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kubadilishwa sawa na kusafisha sajili ya wapiga kura kabla ya kura ya maamuzi kuandaliwa.