Nairobi yapata karani mpya wa bunge


Edward Gichana ameapishwa kuwa karani mpya wa bunge la kaunti ya Nairobi.

Gichana ameapishwa na spika wa bunge la kaunti hiyo Beatrice elachi , siku moja baada ya kuidhinishwa na wabunge wa kaunti, mkao uliozingirwa na utata.

Awali kulikuwa na kioja baada ya spika Elachi kupinga kurejeshwa kazini kwa jacob Ngwele kama karani wa bunge hilo la Nairobi.

Ngwele alikuwa nje ya afisi tangu Novemwa mwaka uliopita baada ya Elachi kuandikia tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC akidai uteuzi wake haukuwa halali.