‘Naibu’ wa soko kukaguliwa


Bunge la kaunti ya Nairobi liko huru kumpiga msasa Anne Kananu Mwenda aliyependekezwa kuhudumu kama naibu gavana wa kaunti.

Hii ni baada ya mahakama kuu kuruhusu hilo alasiri ya leo baada ya kukataa kutoa agizo la kuzuia gavana Sonko dhidi ya uteuzi wake.

Kufuatia uamuzi huo tayari spika Beatrice Elachi amewasilisha jina la Kanuna kwa kamati ya bunge ili kupigwa msasa.