Naibu Spika wa bunge la kitaifa ahusika katika ajali


Mhudumu wa boda boda ameaga dunia na mwenzake kupata majeraha mabaya baada ya kugongwa na gari la Naibu spika wa bunge la kitaifa Moses Cheboi katika barabara ya kutoka Mau Summit kuelekea mjini Molo kaunti ya Nakuru.

Kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru Titus Kizito amedhibitisha ajali hiyo akisema mbunge Cheboi amepelekwa katika hospitali moja mjini Nakuru baada ya kupata majeraha madogo.

Mbunge huyo wa Kuresoi  Kaskazini alikuwa akitoka upande wa Mau Summit  akielekea mjini Molo wakati alipogongana ana kwa ana na piki piki hiyo katika eneo la Casino alipokuwa akijaribu kukwepa shimo katika barabara hiyo.

Mwili wa  marehemu unahifadhiwa katika  hifadhi ya hospitali ya Molo huku mwenzake akiendelea kutibiwa katika hospitali hiyo.