MZOZO WA MPAKA USULUHISHWE BILA MVUTANO


Wito umetolewa kwa viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Taita Taveta na Makueni kusuluhisha tatizo la bila kuchochea wananchi kwanio swala la mpaka limekuwa kwa muda mrefu.
 
Kulingana na wenyeji wa Mtito Andei wanasema lamsingi ni huduma zipatikane kwa mwananchi na wameishi eneo hilo bila ya kugombana kuhusu mpaka huo.
 
Haya yanajiri huku serikali ya kaunti ya Taita Taveta ikidai umiliki wa mji huo licha ya kaunti ya Makueni kusema kwamba hatua ya Taita Taveta kudai umiliki wa mji huo kama uchochezi.