Mzozo unatokota kati ya Kenya na Tanzania


Mzozo unaotokota kati ya Kenya na Tanzania utasababisha hasara kubwa kati ya mataifa haya mawili

Waziri wa Afrika mashariki Aden Mohamed anasema huenda taifa jirani la Tanzania likapoteza zaidi katika mgogoro huu wa kiuchumi

Aidha balozi wa Kenya nchini Tnzania Dan Kazungu anasema mgogoro huu utatafutiwa suluhu, akitoa wito wa utulivu kati ya raia wa mataifa haya mawili

Mzozo huu uliibuka pale Tanzania ilipofunga kabisa mpaka wake baada ya Kenya kupiga marufuku usafiri, ila magari ya mizigo tu