Mwongozo wa mazishi watolewa Elgeyo Marakwet


Onyo limetolewa kwa wakazi wa kaunti ya Elgeyo Marakwet ambao wamewapoteza wapendwa wao kuwa watachukukuliwa hatua kali za kisheria iwapo hawatafanya hafla ya mazishi kabla ya muda wa saa 24 kukamilika.

Kulingana na waziri wa afya katika kaunti hiyo Kiprono Chepkok, wakazi wa kaunti hiyo wana fanya hafla hizo kinyume na maagizo yaliyotolewa wizara ya afya.

Chepkok aidha ametumia fursa hiyo kusisitiza umuhimu wa kuvaa maski akidokeza kuwa watakao feli kutekeleza masharti hayo watakabiliwa vilivyo.

Ameyasema hayo alipokuwa akipokea vifaa mbalimbali vya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa covid 19 kutoka shirika la World Vision viliyogharimu shilling million 1.6