Mwanamume na mganga watiwa pingu Kitui


Mwanamume anayedaiwa kumdhalilisha na kumdhulumu mkewe kwa kumuwekea nta au Glue kwenye sehemu zake za siri akitumia kisu kaunti ya Tharaka Nithi anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo kwa jina James Kifo alikamatwa akiwa mafichoni eneo la Kaningo kaunti ya Kitui akiwa kwa mganga.

Mganga huyo pia ametiwa mbaroni muda mchache uliopita vile vile akitarajiwa kushtakiwa mahakmani baada ya uchunguzi wa kina kukamilika.

Mwanamume huyo wa umri wa miaka 30 alitekeleza unyama huo tarehe 16 mwezi huu wa Mei.

Kukamatwa kwake kumefanikishwa na oparesheni ya pamoja iliyofanywa na maafisa wa DCI kutoka Tseikuru Kitui na wenzao kutoka Tharaka kusini.