Mwanamume katili mahakamani


Mwanamume anayedaiwa kumdhalilisha na kumdhulumu mkewe kwa kumuwekea gundi au Glue kwenye sehemu zake za siri akitumia kisu kaunti ya Tharaka Nithi amepelekwa katika rumande katika gereza la Embu GK hadi tarehe 19 mwezi ujao mahakama itakapotoa uamuzi wa ombi la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.

Mwanamume huyo kwa jina James Kifo anatarajiwa kufikishwa pia katika hospitali kuu ya Chuka kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu , uamuzi ambao umetolewa na Hakimu mkaazi Njoki Kahara.

Kifo alikamatwa hapo jana akiwa mafichoni eneo la Kaningo kaunti ya Kitui akiwa kwa mganga.

Mwanamume huyo wa umri wa miaka 30 alitekeleza unyama huo tarehe 16 mwezi huu wa Mei.