MWANAMUME AZAMA BAHARINI LAMU.


Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 25 amefariki baada ya kuzama bahari Hindi katika eneo la Bandari Salama wadi ya Hindi kaunti ya Lamu

Marehemu Emmanuel Furaha  Karissa alikuwa ameandamana na  wenzake kwenda kuvua samaki ambapo uvuka mkondo wa bahari na kwenda kuvua samaki mbele,wakati wakivuka mkondo huo tena ili kurudi  nyumbani maji yalikuwa yamejaa kabla ya kumshinda nguvu na kisha kumsomba.

Mwakilishi wa afisi ya Seneta katika eneo la Hindi Samy Apolo  amethibitisha tukio hilo akisema Marehemu Furaha ni msaidizi katika afisi ya mwakilishi wadi ya Witu MCA Jonathan Mketa

Kwa sasa mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya Mpeketoni kabla ya kufanyiwa mazishi nyumbani kwao.

Mwili wa mwendazake umepatikana na wananchi walioenda baharini ili kumsaka kwa zaidi ya masaa 11..