Mwanamume amuua kwa kumkata mkewe Makueni


Maafisa wa polisi eneo la Nthongoni Kibwezi kaunti ya Makueni wanamtafuta mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumkata kwa kutumia panga usiku wa kuamkia leo.

Mshukiwa anaarifiwa kutoroka akiwa na panga aliotumia kutekeleza mauaji hayo katika kijiji cha Kongo kaunti hiyo ya Makueni.

Mwili wa marehemu umechukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Makindu kaunti hiyo.