MWANAMUME AKAMATWA KWA KUHUSIKA NA MAUWAJI-TAITA TAVETA.


Maafisa wa upelelezi eneo bunge la Wundanyi wanamzuilia mshukiwa wa mauwaji ya mwanamke wa umri wa makamo ,aliyepatikana ameuwawa huku mikono,miguu na kichwa ikikosekana.

Mwanamume huyo ambaye ni mfanyikazi wa shambani amekamatwa hii leo ,na anaendelea kuzuiliwa katika kituo hicho akitarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho.

Tayari makundi ya kijamii yamekashifu mauwaji hayo ambapo viungo vya mwili ,ambavyo vilikatwa vilipatikana vimezikwa kando ya mto.

Haya yanajiri huku upasuaji wa mwili wa mwanamke huyo ,ukifanyika katika hospitali ya Wesu eneo bunge hilo la Wundanyi.