Mwanamume afariki dunia katika ajali Kirinyaga


Wakaazi wanaoishi karibu na barabara kuu ya Mwea-Embu kaunti ya Kirinyaga wanaisihi mamlaka ya kuangazia barabara kuu nchini KenHA kuweka matuta ya kuthibiti kasi ya magari yanayodaiwa kusababisha ajali za kila mara barabarani eneo la Kimbimbi.

Wakaazi hao wamelalamikia omngezeko la visa vya ajali, cha hivi punde kikiwa jioni ya jan ambapo mhudumu wa bodaboda aligongwa na matatu iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi.

Maafisa wa trafiki kaunti hiyo wanasema kuwa mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Kerugoya matatu na pikipiki zikipelekwa katika kituo cha polisi cha Wang’uru.