MWANAMUME AFARIKI BAADA YA KUHUSIKA KATIKA AJALI -TANA RIVER.


Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 afariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani eneo la Makutano, viungani mwa mji wa Hola kaunti ya Tana River.

Mwendazake ambaye jina limebanwa kwa sasa kwa kuwa familia yake bado haijajulishwa, amefariki wakati akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa mjini Hola ,huku polisi wakisema huenda amepata majeraha ya viungo vya ndani mwilini.

Kulingana na Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Tana River, Patrick Kafulo, mwendazake alikuwa na mwenzake wakitoka upande wa Garsen kuelekea Hola ,kabla ya gari walimokua kupata ajali na kubingiria mara kadhaa ,huku chanjo cha ajali hiyo ikiwa bado hakijabainika.

Mtu mwengine wa pili ambaye amekuwa katika gari hilo ,anaendelea kupokea matibabu katika hospitali hiyo ya Hola.