Mwanaharakati Okiya Omttatah amshtaki gavana Samboja.


Mwanaharakati Okiya Omttatah amefika mahakamani na kuwasilisha kesi ya kupinga kuwa mamlakani kwa gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja akidai hana makaratasi halali ya kuwa uongozini, juma moja tu baada ya mahakama kuu kutupilia mbali kesi kama hiyo kwa kukosa ushahidi wa kutosha.

Kulingana na Omtatah mnamo mwaka 2017 tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC iliifahamisha tume ya kutathmini mipaka na uchaguzi IEBC kwamba, gavana Samboja ana vyeti ghushi ikiwemo shahada.