Mwanafunzi azama baharini Lamu.


Biwi la simanzi limetanda katika shule ya msingi ya Kiongwe Mpeketoni kaunti ya Lamu baada ya mwanafunzi wa darasa la saba kufariki baada ya kusombwa na maji ya bahari alipokuwa akiogelea katika Mkondo wa Eka.

Kulingana na mwalimu wa shule hiyo Madam  jane Karaya marehemu Peter Gungi alikuwa ameandamana na wenzane watatu kwenda baharini kuogelea kama kawaida yao  kabla maji kuwazingira na kumsomba.

Madam Karaya amemtaja mwanafunzi huyo kuwa mwanafunzi bora darasani akisema kwenye mtihani wa majaribuo waliofanya hivi maajuzi maremu aliweza kuibuka nambari moja.

Juhudi za wenzake kumsaidia marehemu baada ya kuzama hazifaulu kwani maji yalikuwa mazito kabla ya kurudi kijijini kuharifu wakaazi kuhusiana na kuzama kwa mwenzao.

Aidha kwa sasa mwili wa mwanafunzi huyo ambaye ni mkaazi wa Ngoi-Tewe- Mpeketoni umehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya Mpeketoni.