Mwanafunzi afa majini Busia


Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Bugisa Lokesheni ya Bunyala mashariki, eneo bunge la Budalangi kaunti ya Busia baada ya kijana
mmoja mwanafunzi wa darasa la nane kuaga dunia alipokuwa akioga ndani ya kidimbwi cha maji.
kidimbwini.

Marehemu Jonathan Were aliye na umri wa miaka 18 mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya msingi ya Sifugwe,alikuwa akiogelea na wenzake wawili kabla ya kupoteza maisha kutokana na wingi wa maji.

Chifu wa lokesheni hiyo Tom Mudonga aliyethibitisha kisa hicho ameshauri wazazi kuwa waangalifu na watoto wao hasa wakati huu ambao
wako nyumbani kwa likizo ndefu.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Port Victoria polisi wakiendeleza uchunguzi.