MWADIME KUHUSU USHIRIKIANO WA VIONGOZI- TAITA TAVETA.


Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime ametoa wito wa ushirikiano baina ya viongozi mbalimbali wa kisiasa, kaunti ya Taita Taveta.

Akiongea wakati wa hafla ya shukrani baada ya kuhusika katika ajali mwaka jana,Mwadime anasema siasa za chuki hazina msingi na sharti wananchi wawe makini na viongozi wanaotoa cheche za maneno.

Mwadime aidha amesema wakati umefika kwa viongozi kaunti ya Taita Taveta kuweka kando tofauti zao ,na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.