MVURYA NA SAMBOJA WATEUA JOPO LA KUSULUHISHA MZOZO WA MPAKA.


Serikali ya Kwale na ile ya Taita taveta wameteuwa jopo litakaloshughulikia swala tata la utatuzi wa mzozo sugu wa mpaka kati ya kaunti hizo mbili .

Gavana wa Kwale Salim Mvurya anasema kwamba jopo hilo, litakaloongozwa na waziri wa ardhi wa kwale Saumu Beja Mahaja, liko na siku 30 za kuchukua maoni ya wakaazi wa maeneo ya mpakani ,ili kutoa mwafaka wa suluhu la mzozo huo.

Kwa upande wake gavana wa Taita taveta Granton Samboja , amesema wakaazi wa eneo hilo la mpakani hukumbwa na changamoto za kimsingi kutokana na mzozo huo.