Muhuri yahofia zoezi la ukusanyaji sahihi la BBI.


Huku uzinduzi wa zoezi la kukusanya sahihi kwenye ripoti ya BBI ukitarajiwa kufanyka hii leo jijini Nairobi, shirika la kutetea haki za binaadam la MUHURI linahofia kwamba huenda zoezi hilo likachangia kusambaza virusi vya corona kwa wananchi.

Kwenye taarifa vya vyombo vya habari mwenyekiti wa shirika hilo Khelef Khalifa anasema kwamba zoezi hilo lingesitishwa kwa muda na kisha hela zilizotengewa zoezi hilo kusaidia kwenye juhudi za kupambana na ugonjwa wa Covid19 unaozidi kuangamiza wananchi.

Khalifa anasema kwamba maswala yalioyotajwa kwenye ripoti hio ikiwemo kupambana na ufisadi, nafasi za ajira kwa vijana, akinamama na walemavu sawia na suala la ubaguzi wa kikabila na kutengwa kwa jamii sio maswala ya dharura ikilinganishwa na janga la corona.

Haya ameyasema licha ya kamati inayosomamia ripoti hio ya BBI kushikilia kwamba zoezi hilo litatekelezwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za kudhibiti msambao wa ugonjwa wa covid 19.