Mudavadi ataka mgombea wa “Handshake” Matungu


Kinara wa ODM Raila Odinga amemtaka rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga kutokuwa na mgombea katika uchaguzi mdogo eneo bunge la Matungu kupitia vyao.

Mudavadi ansema kuwa hatua hiyo itakuwa ishara tosha kuwa anaunga mkono BBI kikamilifu hivyo basi wanafaa kumuunga mkono mgombea wa ANC katika uchaguzi huo mdogo.

Amesema haya katika makao makuu ya chama hicho cha ANC katika hafla ya kumkabidhi Oscar Peter Nabulindo tiketi ya kuwania kiti cha ubunge katika uchaguzi huo wa mwezi Machi mwaka ujao.