MUATHIRIKA WA CORONA ATOROKA


Hali ya taharuki imetanda miongoni mwa wakaazi wa kijiji cha Hindi kaunti ya Lamu baada ya muathirika wa virusi vya korona kutorokea eneo hilo..

Muathirika huyo mwenye umri wa 22,alitakikana kufika katika hospitali kuu ya Rufaa ya King  Fahad iliyoko Kisiwani Amu ili kutengwa kabla ya kuamua kutoroka.

Katika kutoroka kwake,muathirika alipanda boti kutoka Kisiwa cha Amu hadi Mokowe,na alipofika Mokiwe alihabiri Probox iliyomfikisha eneo la Hindi na kuingia hotelini huku wakaazi wakisema kwamba ametangamana na watu wengi katika eneo hilo la Hindi.

Muathirika huyo ambaye ni mkaazi wa Langoni Kisiwani Amu ni miongoni mwa watu wawili walioripotiwa kuwa na virusi vya korona hapo jana na Wizara ya Afya nchini.

Waziri wa Afya Lamu Ann Gathoni amethibitisha kutoweka kwa muathirika akisema maafisa wa Afya wanamfatilia ili kuweza kumnasa na kumtenga .