Mtoto anyongwa na kamba ya bembea Jomvu.


Mtoto mwenye umri wa miaka minne ameaga dunia baada ya kudaiwa kunyongwa na kamba ya bembea aliyokuwa akicheza nayo katika mtaa wa Kwa Mwanzia Kwenye eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa.

Akidhibitisha kisa hicho afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Alfred Nthiga amesema kwamba mtoto huyo aliyekuwa akicheza na wenzake ni kana kwamba aliteleza kwenye bembea hio na kisha kunaswa shingoni na kamba iliyomnyonga.