Mtambo wa hewa ya oxygen kukamilika Taita taveta .


Kamati ya bunge la kaunti ya Taita Taveta kuhusu afya imesema kwamba mtambo wa hewa ya Oxigeni itakamilika chini ya kipindi cha majuma matatu yajayo.

Kulingana na mwenyekiti wa kamati hiyo Omar Ahmed anasema mtambo huo ulikua umekwama baada ya mwanakandarasi kukosa kulipwa fedha zake kima cha shilingi milioni 2.6.

Omar anasema mtambo huo utapiga jeki sekta ya afya ambayo kwa sasa hutegemea oxigeni kutoka kaunti ya Mombasa.