MSHUKIWA WA VIRUSI VYA CORONA RAIYA WA UTALIANO APATIKANA BILA VIRUSI -LAMU.


Hatimaye Raia Mtaliano ambaye alikuwa mshukiwa wa virusi vya Korona katika eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu amepatikana Negative pasipo kuwa na virusi vya Korona kama ilivyoshukiwa.

Kamishna wa kaunti ya Lamu Irungu Machari amesema kaunti Lamu imekuwa na visa viwili washukiwa wa Covid 19 ambao vipimo vyao vilipelekewa kwa uchunguzi zaidi na wote wamepatikana bila Virusi hivyo vya Korona.

Macharia amehuzunishwa na tukio lililoteka hivi maajuzi wakati raia huyo Mtaliano alipofikishwa Kisiwani Amu ili kutengwa katika hospitali kuu ya King Fahad ili kusubiri vipomo vyake vya damu ambapo wakaazi walidinda asishukishwe kwenye boti kwa hofu ya kuambukizwa Korona.