Mshukiwa wa mauaji Kirinyaga kuzuiwa kwa siku 10


Mwanamume wa miaka 34 aliyekamatwa kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake na kumzika kwake huko Kirinyaga atazuiwa na polisi kwa siku kumi

Ndio uamuzi wa mahakama ya Kerugiya kupitia hakimu mkuu mkazi, Grace Kirugumi, ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi

Mkuuu wa upelelezi katika kesi hiyo Richard Nyakora anasema katika muda huo wa siku 10, upasuaji utafanyiwa maiti ya mwanamke huyo, huku naye mshukiwa Murimi Wanjohi, akitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili

Mapema leo, mkuu wa polisi eneo la Kirinyaga ya kati Daniel Ndege alisema mshukiwa aliyekamatwa huko Nbaricho eneo bunge la Ndia alidai kuchochewa na kuabudu shetani kuttekeleza mauaji hayo