MSHUKIWA ATOROKA KATIKA KITUO CHA POLISI ,BAADA YA KUMRUSHIA ASKARI KINYESI,TANA RIVER.


Polisi mjini Bura kaunti ya Tana River wanamsaka mshukiwa mmoja ambaye ametoroka katika kituo cha polisi cha Bura, baada ya kurushia askari kinyesi kwa uso mapema leo.

Mshukiwa huyo ambaye amekuwa akizuiliwa katika kituo hicho kwa kosa la kupiga mwengine, ametoroka wakati ambapo amesindikizwa hadi chooni kujisaidia.

Kamanda wa polisi Tana North, Benedict Mwangangi, anasema wakati askari wa zamu alipoona mshukiwa anachelewa kutoka chooni, ameenda kugonga mlango huo ,na ndipo hapo mshukiwa amemrushia kinyesi usoni na kisha kutoroka.

Mwangangi na maafisa wengine kwa sasa, wanaendeleza juhudi za kumsaka mshukiwa huyo katika vichaka vinavyozunguka mji huo wa Bura.