MSHUKIWA ALIYEPATIKANA NA NA NYOKA LIKONI MOMBASA AKIRI KOSA HILO MBELE YA MAHAKAMA


Mahakama ya Mombasa hapo kesho inatarajiwa kusikiliza kesi kuhusu mshukiwa Benedict Karisa Fondo anayekabiliwa na mashtaka ya kufumaniwa na mnyama mwitu ambaye ni Nyoka aina ya Chatu bila kibali maalum.

Mahakama imearifiwa kwamba mshukiwa alipatikana na nyoka huyo mwenye urefu wa futi 2 nukta 3 na mwenye uzani wa takriban kilo kumi katika kivuko cha likoni Ferry alipokuwa akijaribu kuvuka ferry kutoka kisiwani kuelekea Likoni.

Mshukiwa huyo amekiri kosa hilo mbele ya hakimu Vincent Adet aliyeagiza azuiliwe hadi hapo kesho baada ya afisa anayechunguza kesi hio kuomba muda wa kufanya marekebisho ya jina la Mshukiwa kwani majina yaliowasilishwa mahakamani hayakuambatana na yale yaliokuwa kwenye kitambulisho chake.

Kesi hio itaendelea hapo kesho.