MIKAKATI MIPYA YA CORONA TANA RIVER.


Kamati ya dharura ya kupambana na maswala ya corona kaunti ndogo ya Tana Delta yasema kwamba italazimika kuchagua tena vituo ambavyo vitatumika kama karantini dhidi ya ugonjwa wa corona ,hasa baada ya shule kufunguliwa.

Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Tana Delta, William Nasongo, ameongoza mkutano wa washikadau kutathmini upya matayarisho ya eneo hilo dhidi ya ugonjwa wa corona, huku swala la karantini likijitokeza kwani vituo vya hapo awali vya Garsen High na Tarasaa ,haviwezi kutumika baada ya shule kufunguliwa.

Nasongo amehimiza viongozi wa kidini kuwa msitari wa mbele ,kuhakikisha itifaki za kuzuia ugonjwa wa corona zinazingatiwa hasa katika sehemu za ibada , hafla za mazishi au harusini.