Miili yapatikana ikioza Kilifi.


Kamati ya usalama kule Kilifi kusini inachnguza kisa ambapo  miili ya wanawake wawili  imepatikana wakioza katika kichaka kimoja eneo hilo.

Maiti za wawili hao zilipatikana zikioza katika msitu mmoja kwenye barabara ya kuelekea chou cha mafunzo ya utalii cha Ranarld Ngala.

Kulingana na Chifu wa eneo hilo David Kahindi mauwaji ya wawili hao yalitokea katika mazingira tata na kwamba serikali inafanya kila iwezalo kutegua kitendawili cha mauwaji hayo.

Inaarifiwa kuwa eneo hilo pia hushirkishwa na maswala ya upigaji mtindi kwa wingi na kwamba ni hali ambayo imesaabisha ukosefu wa usalama.

Afisaa huyo wa utawala amefichua kuwa maafisa wa usalama wamelizamia swala hilo na kwamba litafchuka hivi karibuni.