Mgonjwa aaga dunia katika ajali ya ambulensi


Mtu mmoja ambaye alikua mgonjwa akisafirishwa kwa Ambulensi kutoka hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi kaunti ya Taita taveta hadi hospitali ya ukanda wa pwani Mombasa ameaga dunia baada ya gari hilo la kubeba wagonjwa kuhusika katika ajali.

Inaarifiwa dereva wa gari hilo alipoteza mwelekeo na kubingirika mara kadhaa katika eneo la Ndara barabara kuu ya Nairobi -Mombasa na mgonjwa huyo akafariki dunia aliporudishwa katika hospitali ya Moi akiwa na shida ya kupumua.

Dereva wa gari hilo,muuguzi sawa na jamaa ya aliyefariki dunia wamepata majeraha na sasa wanatibiwa katika hospitali ya rufaa ya Moi huku polisi wakianzisha uchunguzi wa kina.