Mgomo wa madaktari Migori waingia siku ya 20


Huduma za matibabu katika hospitali za umma kaunti ya Migori zinaendeela kutatzika kutokana na mgomo wa madaktari ambao umeingia ya 20 hii leo.

Madaktari hao wakiongozwa na mwenyekti wa chama cha madaktari nchini tawi la Nyanza Kevin osuri wameapa kuendelea na mgomo hadi pale maslahi yao yatakapoangaziwa kikamilifu kuu ikiwa bima ya matibabu.

Kauli yake imeungwa na katibu wa chama hicho eneo hilo Dr.Lameck Omweri

Hata hivyo, afisa mkuu msimamizi wa afya kaunti ya Migori Dk Isca Oluoch amewahimiza madaktari hao kurejea kazini kw amisingi kuwa kaunti inashughliokia bima zao za matibabu.