Mgombea wa eneo bunge la Msambweni ODM awasilisha stakabadhi zake.


Wagombea Omari Boga odm,shehe Mahmoud wa wiper pamoja na hamisi mwakaonje wa United green movement wanatarajiwa kuwasilisha stakabadhi zao kwa tume ya uchaguzi na mipaka nchini iebc ili kuidhinishwa kuwania ubunge wa msambweni katika uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe 15 December mwaka huu

.

Mgombea wa odm Omar boga anatarajiwa kuandaa mkutano mkubwa wa kisiasa akiandamana na gavana wa kuanti ya Mombasa Hassan joho pamoja na wabunge 20 kutoka Chama Cha odm.

Ziara ya Wana odm inajiri siku tu baada ya mrengo tangatanga kukita kambi katika msambweni kumpigia debe mgombea huru Feisal Abdallah