Mfichuzi wa sakata ya Covid-19 Millionaires, Otieno Agutu akamatwa kwa utapeli


Maafisa wa polisi wa idara ya upelelezi DCI wanawazuia washukiwa watatu waliomteka nyara mfanyabiashara kwa lengo la kumpora pesa

Kwa mujibu wa DCI, washukiwa hao walimuitisha hongo ya shilingi milioni mbili mkurugenzi wa kampuni ya Hi-tech wakijifanya kuwa maafisa wa EACC na KRA

Watatu hao, Godwins Otieno Agutu, Alex Mutua Mutuku na Ken Gichovi Kimathi walimhangaisha mkurugenzi huyo kwa madai ya kukwepa kulipa ushuru

Walifika ofisini kwake tarehe 26 mwezi ulipota na kuondoka na kipakatalishi chake kabla ya kumuandama hadi nyumbani kwake tarehe 29 na kuondoka na shilingi nusu milioni

Wengine watatu wanaosakwa ni maafisa wa KRA, Houdouvia Njoroge, Harrison Ochar and Brian Kimemia.