MCHUJO WA ODM MSAMBWENI KUPITIA KURA YA MAONI


Kinara wa ODM Raila Odinga amesema kwamba watachagua atakayepeperusha bendera ya ODM katika uchaguzi mdogo wa msambweni kupitia kura ya maoni ili wapate mgombea aliye na umaarufu ili kuhifadhi kiti hicho.

Kinara huyo ameafiki kuwepo na dosari katika michujo ya wagombea wa viti mbali mbali katika uchaguzi mkuu uliopita Hali ambayo ilisababisha chama hicho kupoteza viti vingi katika uchaguzi mkuu uliopita

Raila aliyekuwa akizungumza na wagombea wa kiti Cha ubunge Cha msambweni huko ukunda kaunti ya kwale ,kilichowachwa wazi na mwendazake Suleiman  Dori miezi sita iliyopita amesema kwamba ni sharti kiti cha ODM kihifadhiwe katika eneo bunge hilo la msambweni huku akiwataka wafuasi wa ODM kumuunga mkono kikamilifu mgombea atakayechaguliwa.

Kwa upande wake naibu kinara wa ODM aliyepia gavana wa mombasa Ali Hassan Joho amewahakikishia wagombea hao mchujo ulio na uhuru na haki.

Hadi kufikia sasa ODM iko na wagombea wanne Omari Boga,Sharlet Mariam, Nicholas zani,feisal Dori.