MBUNGE WA MALINDI AISHA JUMWA AKOSOA RIPOTI YA BBI KWA MADAI YA KUWAHADAA WAKENYA.


Hisia mesto zingali zinatolewa kuhusu ripoti ya BBI huku kinara wa chama cha ODM Raila Odinga akidaiwa kutumia fursa hiyo kuwahadaa wakenya.

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ameikosoa ripoti hiyo ,kwa misingi kuwa imekiuka mapendekezo ya wakaazi wa pwani.

Jumwa alikuwa akizungumza katika halfa ya mazishi huko Jilore , na kuwataka wakaazi wa eneo hilo na wakenya kwa ujumla kuisoma na kuielewa ripoti hiyo badala ya kushurutishwa.

Kulingana na Jumwa nakala za ripoti hiyo hazijawafikia wakaazi wa mashinani ,hivyo kuifanya vigumu kwao kuisoma ripoti hiyo.

Jumwa amepinga kuongezwa kwa mgao wa fedha za kaunti kutoka asilimia 15 hadi 35 ,kwa misingi kuwa ugavi wa mapato huenda ukabadilika kulingana na idadi ya watu.

Kauli ya Jumwa inakinzana na ya viongozi wengi Pwani, ambao wanaunga mkono mchakato huo.