Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa aachiliwa kwa dhamana.


Mahakama kuu ya Mombasa imemuachilia kwa dhamana ya shillingi millioni 2 au shillingi millioni 4 na mdhamini wa kiasi sawia na hicho mbunge wa Malindi Aisha Jumwa.

Pia imemuachilia kwa dhamana ya shillingi millioni 1 na mdhamini wa kiasi sawia na hicho au pesa taslimu shillingi millioni moja unusu mwenzake Geoffrey Otieno.