MBUNGE WA KINANGO ,KWALE ASEMA KUUNDWA KWA CHAMA PWANI KUTASADIA ENEO HILO KIMAENDELEO.

Mbunge wa kinango Benjamini tayari amesisitiza kuwa kama wabunge wa pwani wakiwemo maseneta wanalenga kuunda chama cha kisiasa watakachotumia katika uchaguzi mkuu ujao kwa kile wanachodai kuwa eneo la pwani limekua likitengwa kimaendeleo tangu jadi
Kauli ya tayari inajiri wakati kaunti 6 za pwani zitapunguziwa mgao wao wa kifedha kwa Zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mujibu wa mapendekezo ya tume ya ugavi wa mapato nchini
Tayari aliyekua akizungumza na wanahabari kule kinango amemshtumu vikali chama cha odm kwa kile anachodai kuwa kiliwatenga wabunge wa pwani katika nyadhifa za kamati za bunge la kitaifa na seneti licha ya pwani kupigia kura chama cha odm kwa Zaidi ya asilimia 70 katika uchaguzi mkuu uliopita
Vile vile tayari ametaja umuhimu wa kuwa na chama kiasiasa pwani akisema kuwa itasaidia ukanda wa pwani kupata ugavi sawa wa rasilimali kama maeneo mengine nchini