Mazishi bila mwili


Familia moja katika eneo la Ndenderu, kaunti ya Kiambu, imelazimika kuandaa ibada ya mazishi bila ya kuwepo maiti ya mwana wao aliyeaga dunia kwani maiti inazuiliwa na hospitali ya Getrudes.

Hii ni baada ya familia hiyo kushindwa kulipa shilingi milioni 13 wanazodaiwa na hospitali hiyo.

Mtoto huyo Brian Kimani, aliye na umri wa miaka 13 alifariki wiki chache zilizopita alipokua akitibiwa saratani hospitalini humo.

Gharama ya matibabu yake ilikua shilingi milioni 18 na familia hiyo ikaweza kulipa shilingi milioni nne.

Usimamizi wa hospitali ya Getrudes unashikilia kwamba ni sharti walipe pesa zote ili waruhusiwe kuchukua mwili wa Brian kwenda kuzika, hali ambayo imelazimu familia kufanya ibada ya mazishi bila mwili ili kumuaga Brian.